News / Habari
 
Balozi Dola & SUGU a.k.a Mr. II US Tour
 
 
 
ABOUT THE KILLING OF NELSON RUTTA
(FAZA NELLY FROM X PLASTAZ)
by Thomas Gesthuizen, April 5, 2006

In this short overview I will try to summarize some of the facts
surrounding the tragic and sudden death of Faza Nelly, one of Africa's hip
hop heroes and an icon in his local scene of Arusha, northern Tanzania.

On Monday 27 March, emcee Faza Nelly (Nelson Chrizostom Rutta) from
Arusha, Northern Tanzania was stabbed 9 times with a knife by his
neighbour.
Two days later he died from the results of the stabbing as the knife had
severely damaged his longs.

Faza Nelly was a member of X Plastaz, a rap group of six from Arusha whose
work is known worldwide through their concert tours to places such as
Brazil, UK and Holland, an album released worldwide and tracks which
appeared on compilations such as the Rough guide to African Rap. The group
became popular through their own brand of East African hip hop, which is a
merger of hardcore beats, Swahili rhymes and traditional acappella Maasai
music sung by a Maasai warrior who spends most of his time in a
traditional environment on the Maasai steppe.

THE MURDER
Nelly was murdered by Moses Yohana Kilevo, a neighbour who had been
terrorizing his neighborhood for some time with inappropriate behavior
such as writing 'I am a killer' on the walls of his shared compound, which
was also home to neighbour' kids. This behavior had caused the
neighbours to sign a petition to evict him, but to no avail. When Musa,
one of Nelly's friends who lived in the same house, tried to talk to
Moses, he was arrested by police for false robbery charges - it was Moses
who had sent this complaint.
Nelly tried to get Musa out of jail and talked to the police who asked him
to return with neighbours to testify, then he went home to try to talk to
Moses.
Moses however got angry and wanted to fight Nelly, who then decided to
evade problems and go back to his own room. Seconds later, Moses came out
of his room with a big rambo knife and stabbed Nelly 9 times in several
places including his nose, armpits and lungs.
There was never a fight, and Nelly according to his family and environment
was a totally peaceful person who would never harm anyone, he showed
compassion to the 'have-nots' of society as can be heard in his lyrics
such as 'Nini dhambi kwa mwenye dhiki'. Also in this case he could not
even defend himself against the attack from the back.
Nelly spent 2 days in hospital where he was put to a breathing machine. He
had surgery two times, but after the second time his condition suddenly
dropped and he died in the presence of doctors and his friend Musa.

THE KILLER - REWARD OF 500.000 TSH
The killer, Moses Yohana Kilevo, was a regular person with a family (wife
and 2 kids), other than what was mentioned in the Tanzanian press before,
he was not a 'kichaa' (insane). However he was known to be a rude and
unpleasant person to his neighbourhood. Moses fled away after stabbing
Nelly and has not been seen again. Arusha police are investigating and
chances are that he may have fled to Nairobi where he has relatives. A
reward for bringing the killer out has been put up by the family to the
value of 500.000 Tanzanian shillings. See attached photo.

THE FUNERAL
Because the family wanted to wait until Nelly's brother Godson (Gsan, also
a member of X Plastaz) returned from Chicago along with his wife and X
Plastaz manager Thomas Gesthuizen (J4), the 'matanga' (mourning ceremony)
took four days, and Nelly was buried on the fifth day.
The mourning attracted hundreds of youth and elders from Arusha and
beyond, including Kamaa from Kalamashaka and Black, another Kenyan emcee.
The funeral itself took place in Njiro (Arusha) and attracted over 1000
attendants: 40 dala-dala's (matatus) had to be used to carry everyone who
didn't have their own transport.

WHAT'S NEXT FOR X PLASTAZ
At present it's not sure how X Plastaz as a group will continue on. Most
likely the emcees will continue the work set out by Nelly; a vision of
spreading conscious lyrics, 'healing society' as Nelly would say, while
entertaining at the same time.
X Plastaz had just finished a new music video: 'Nini dhambi kwa mwenye
dhiki' which was a solo track by Nelly about the fate of poor people in
Tanzania. The video shows him in Unga Limited, a local Arusha getto, in
the Maasai steppe around Mto wa Mbu, and on top of Ol Doinyo Lengai, an
active volcano which is the 'Mountain of god' to the Maasai people in the
area. The video was released to Tanzanian television on the day of the
burial.
They were also about to release a cd-single of the track 'Hiyo' which can
be listened to online at www.myspace.com/xplastaz

MORE INFO, CONDOLENCES AND PHOTOS
More info can be found at www.xplastaz.com - there is also a condolence
register which has been signed by over 100 people from around the world.
Photos of the burial, and the new video 'Nini dhambi kwa mwenye dhiki'
can be seen online soon.
_____________________

END OF PRESS RELEASE, NOT FOR PUBLICATION:
contact x plastaz: Thomas Gesthuizen (J4), email: rahh@xs4all.nl

 
March 30, 2006
 
News article from DJ Jumanne (J4): Africanhiphop.com
Sad news from Tanzania where Faza Nelly, one of the founding members of Tanzanian rap group X Plastaz, passed away last night. Nelly had been admitted to hospital with wounds inflicted by a knife that a psychotic neighbour had used to attack him. Doctors had hope of curing him, but the damage to his lungs proved too severe.

Nelly's death has shocked his family, friends and the international music community who have expressed their grief in the condolence register at the
X Plastaz website. He will be buried the coming weekend and his brother and group member Gsann will come over from the USA to attend the funeral.
 
With the passing of Nelly, the hip hop community has lost a modest but highly skilled emcee whose lyrics were tales from the grassroots of society. He showed a great respect for the natural treasures of Tanzania and for traditional culture, such as in the song 'Aha' (see video here). Nelly truly cared for the community and the poor & helpless and was never tempted to go with the trend of Tanzanian rap to become more commercial and less about the hardships of the common people. At the same time he knew how to enjoy life and his sense of humor never failed to break the ice with people from all over the world.

In his travel with the group he got to see different parts of the world such as Belgium, UK and Brazil. He was booked to perform in Gabon (West-central Africa) in early June, and a music video featuring him rapping on top of the holy mountain of the Maasai (the active volcano Ol Doinyo Lengai) was about to be released in Tanzania along with the new single 'Hiyo' which is also on the new Kunta Kinte Clothing mix tape (see the
X Plastaz Myspace page for audio).

Africanhiphop.com would like to send condolences to his family, friends, colleagues and fans.
More news soon as Africanhiphop.com editor Juma4 will also be in Tanzania the coming week.
 
August 31, 2005
 
DONDOO za BONGO Na Jasmes Nindi,Tanzania
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
R.I.P COMPLEX - LALA MEMA PEPONI MWANANGU
 
 
MTAYARISHAJI mahiri wa muziki katika studio mpya na za kisasa nchini Tanzana, Saimon Sayi,"Complex"

amefariki katikati ya mwezi Agosti eneo la Mbwewe,Tanga akiwa njiani kuelekea Arusha.

 
Complex,ambaye binafsi nilianza kufahamiana naye kupitia msanii,Ambene Yessaya"AY"

 akiwa produza katika studio za Backyard wakati huo,alipatwa na mauti hayo akiwa

njiani kuelekea Arusha akitokea mjini Morogoro katika tamasha la Fiesta.

 
Ajali hiyo ambayo ilisababisha vifo vya watu kadhaa ambao walikuwemo

ndani ya gari aina Toyota Landcruiser iltokea katika eneo hilo

baada ya gari hiyo kupasuka gurudumu la nyuma na kupinduka ambapo

Complex na mpenzi wake Viviani Tilya ambaye alikuwa mytangazaji wa kituo cha redio

 Clouds FM cha Dar es Salaam,Tanzania walifariki.

 
Complex anakumbukwa na wadau wa muziki katika mchango

wake mkubwa hasa pale alipo mpa tafu Ambene Yessaya"AY"

katika kibao chake  NI Raha tu ambacho kilitokea kupendwa.

 
Mbali na kushirikisha katika kibao hicho,pia Complex aliweza kusikika

katika vibao kdhaa vya wasanii kikiwemo,.Taifa la Bongo kilichofanywa

na kundi la B-clan ambacho kiliwashirikisha wasanii kama Suma Lee,Noorah,Complex na wengineo.

 
Mbali na kibao hicho,Complex kuonekana akiwa katika kiitikio,pia

aliweza kushirikishwa katika kibao cha Nyamaza ambapo wasanii  Dataz na Sguezer wamepata lifti yake.

 
Mbali na kazi hizi ambazo amezitoa siku za karibuni,pia ameweza kurekodi

albamu za wasanii wengi walikwemo Kundi la Wagosi wa Kaya,albamu yao mpya "Nyeti" ni matunda ya Complex.

 
Binafsi,nilikutana naye wiki moja kabl ya kifo chake,nilifika kazini kwake majira

ya saa nane mchana,alinipokea vizuri sana kama kawaida yake.

 
"Ndiyo mzee,karibu bwana,tunafanya marekebisho makubwa katika studio

yetu ndio maana nipo katika chumba ambacho hujaoea kunikuta" alisema huku

akiwa na wasaniiwa kundi la Ghetto Boyz.

 
Hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya mwisho kuonana na msanii huyo.
 
Complex alizaliwa mwaka 1978 na kpata elimu yake katikashule

mbalimbali hadi alipomaliza masomo yake ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Popatlal,Tanga Tanzania.

 

 +++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Ghetto Boys kuzinduwa - Yote Bure

 
KUNDI la muziki wa hiphop la Ghetto Boys limekamilisha kurekodi albamu yake

 mpya iliyobeba jina la Yote Bure. Akizungumza na Mtandano huu,Tanzania jana,mmoja

wa wasanii wa kundi hilo,Juma Mjivuni alisema albamu yao hiyo imebeba jumla ya nyimbo nane.

 
Alisema kazi ya kurekodi albamu hiyo imefanyika katika studio tofauti ambazo ni Aegies,

Sound Crafters,Bongo Records pamoja na Mwingu zote za Dar res Salaam.

 
Msanii huyo aliema baada ya kazi hiyo kukamilika,wanajiandaakufanya uzinduzi wa albamu hiyokatika siku za mbele.
 
Aidha msanii huyo alisema mbali na hilo,Pia kundi lake linajiandaa kufanya

shooting ya video ya albamu hiyo ambapo wimbo mmoja Maisha ya ndoa umeanza kufanyiwa shooting

 chini ya kampuni ya King Kiff ya Tanzania.

 
Kundi hilo limeundwa na wasanii watano ambao wamejiengua kwa msanii Afande Selle ambaye ni mfalme

 wa wakali wa rhymes 2003,.

 
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
August 25, 2005
 
DONDOO za BONGO

Na Jasmes Nindi,Tanzania

Dudu Baya sas yuko kwenye Kiwango

 
MSANII wa muziki wa Bongo fleva,Godfrey Tumaini"Dudu Baya" amekamilisha kazi

ya kurekodi albamu ya sita iliyobeba jina la Kiwango.

 
Akizungumza na mtandano huo,Tanzania jana,msanii huyo alisema kazi hiyo

imekamilika na albamu yake hiyo imebeba jumla ya nyimbo tisa.

 
Alisema katika albamu yake hiyoamewashirikisha wsanii wengi wakiwemo

Joan,Doreen pamojana kundi la kinadada la Unique sisters.

 
Msanii huyo alisema albamu yake hiyo ambayo ni moto wa kuotea mbali imeshaingia katika soko la muziki nchini.
 
Dudu baya alisema baada ya kumaliza kazi ya kurekodi albamu hiyo ameanza kazi ya kufanya shooting kwa albamu nzima.
 
Albamu hiyo imerekodiwa katika studio tofauti za muziki zikiwemo MasterJay na Aegies zote za Dares Salaam,Tanzania.
 
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Rich One - akamilisha album yake - Hakuna Kitu

 
Richard Shauri"Rich One" msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Tanzania amekamilisha kazi ya

kurekodi albamu yake ya pili iliypobeba jina la Hakuna kitu.

 
Akizungumza na Mtandano huu,Dar es salaam Tanzania,hivi karibuni,alisema kazi

ya kurekodi albamu hiyo imefanyika katika studio tofauti Tanzania.

 
Alisema lengo la kufanyia katika studio hizo ni kujaribu kupata ladha

tofauti za muzikitoka kwa watayarishaji wa muziki.

 
Aloizitaja studio ambazo zimerekodi albamu yake hiyo kuwa ni Bongo records,

Home Boyzs ya Kenya,Sound Crafters,Jaysilk.

 
Mbali na hilo,alisema katika albamu yake hiyo ameweza kuwashirikisha

waanii kama Juma Nature,Stara Thomas,Late Viviani Tilya,Jose MtamboRichard Mangustino,

Amani Temba"Mh Temba"Banana Zorro na Mike Tee.

 
Aidha alizitaja nyimbo ambazo zinapatikana katika albamu hiyo kuwa ni

Penzi,Malengo,Na bado,Harusi,Intro,Outro,NimedataBwax,Umenidatisha na uliobeba jina la albamu hiyo Hakuna kitu.

 
Sambamba na hilo,msanii hyuyo alisema ameanza kazi ya kufanya shooting ya albamu hiyo ambapo

 wimbo wake Unanidatisha umefanyiwa na kampuni ya Roca Production ya Tanzania.

 
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
August 19, 2005
 
Ipo Siku album mpya ya Mheshimiwa Temba

MSANII mahiri wa muziki wa bongo fleva Amani Temba"Mheshimiwa Temba" toka
kundi la Wanaume Family ameanza kazi ya kurekodi albamu yake ya pili
iliyobeba jina la Ipo siku.

Akizungumza na Mtandano huu,Tanzania juzi,alisema tayari ameanza kazi ya
kurekodi albamu hiyo ambayo itabeba jumla ya nyimbo kumi.

Alisema nyimbo ambazo tayari amezirekodi ni Kosa la Baba na Namshukuru
ambazo amezirekodi katika studio mbili ambazo ni Sound Crafters na Aeges
zote za Dares Salaam,Tanzania.

Aidha msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na albamu yake ya
kwanza,Umasikini Jeuri alisema albamu yake hiyo itaingia katika soko la
muziki mwaka kesho.

Katika albamu yake hii amewashirikisha wasanii kadhaa wakiwemo Juma
Nature,Luteni Karama pamoja na Chegge wote toka kundi lake la Wanaume
Family.

Msanii huyu kwa sasa amejipatia sifa nyingi kutokana na kibao chake Nampenda
yeye kupendwa na wengi ambacho kipo katika albamu yake ya Umasikini Jeuri.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
Bwana Misosi yuko tayari kutia ndani tena

JOSEPH Rushahu,"Bwana Misosi"msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya
amekamilisha kazi ya kurekodi albamu yake ya pili"Kazi yangu" ambayo imebeba
jumla ya nyimbo nane.

Akizungumza na Mtandano huo,Tanzania juzi,alisema kazi ya kurekodi albamu
yake hiyo imefanyika katika studio tofauti.

Alisema mbali na kufanyiaka katika studio tafauti pia,amewashirikisha
wasanii tofauti ili kuleta ladha tofauti katika albamu yake hiyo ambayo ni
ya pili kwake.

Katika albamu hiyo amewashirikisha wasanii kama Jose Camilione toka Uganda
katika kibao Walisema,Red Sun toka Kenya katika kibao Heshima ambacho
kimeanza kusikika katika vituo vya redio nchini Tanzania.

Mbali na hao wengine walioshiriki katika albamu hiyo ni Suma Lee toka kundi
la Park lane la mjini Tanga,Inspector Harun,Nurueley pamoja na Shakii.

Albamu hiyo imepangwa kuingia katika soko la muziki mwishoni mwa mwezi
Agosti mwaka huu na itasambazwa na kampuni ya GMC.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
Soggy Kuzinduwa album ya nne - March 11

MSANII wa muziki wa Hiphop Tanzania,Anslem Ngaiza"SoggyDoggy" anajiandaa
kutoa albamu yake ya nne Septemba mwaka huu ambayo itabeba jina la March 11.

Akizungumza na Mtandano huu,Tanzania juzi,alisema kazi ya kurekodi albamu
hiyo imekamilika na kinachosubiriwa ni muda wa kuingiza sokoni.

Alisema albamu yake hiyo imerekodiwa katika studio tofauti ambazo ni Serious
Records,Sound Crafters,G2, zote za Tanzania na Turnatables ya Uganda pamoja
na Home Boys ya nchini Kenya.

Mbali na kurekodiwa katika studio hizo,albamu hiyo pia imewashirkisha
wasanii tofauti wakiwemo Rehema Chamamila"Ray C"Dataz,Suma Lee,Q-Chief,Juma
Nature pamoja na D-Knob.

Alizitaja nyimbo ambazo zinapatikana katika albamu hiyo kuwa ni Ndoa,Uko
wapi?,Pamoja,Raisi wa Bongo,Nilikaona mwaka jana,Nataka kujiua na Kj.

Albamu hii inatarajiwa kubeba jumla ya nyimbo kumi ambazo zinatarajiwa
kupendwa na washabikiwa muziki huu hapa nchini.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
Video ya Choka Mbaya, "Yatima" itaonekana ndani ya Luninga hivi Karibuni

KUNDI la muziki wa hiphop la wasichana watano ambao wote ni walemavu,Choka
Mbaya Sisters limekamilisha kazi ya kurekodi video yao mpya Yatima chini ya
kampuni ya Tripol Media ya Tanzania.

Wakizungumza na Mtandano huu,wasanii wa kundi hilo,walisema kazi hiyo
imefanyika mara baada ya kazi ya kurekodi albamu yao"Yatima kukamilika
kurekodi.

Mmoja wa wasanii wa kundi hilo,Lucy Samson"Sweet Sam" alizungumza kwa niaba
ya wenzake,alisema albamu yao hiyo ambayo ni ya kwanza imebeba jumla ya
nyimbo nane.

Alisema katika albamu hiyo ambayo imerekodiwa katika studio za
SoundCrafters,Tanzania imewashirikisha wasanii kadhaa wakiwemo Bizzman
Ntavyo,Juma Nature,Dully Sykes,Mrisho Ferroz na wengineo.

Albamu hiyo imebeba nyimbo kama Nakupenda wewe,Mashabiki,Ndani ya
klabu,Mpenzi wangu,Ukahaba,Rushwa pamoja na wimbo ulibeba jina la albamu
hiyo Yatima.

Kundi hili ambazo limeudwa na akina dada watupu ambao wote ni walemavu,plipo
chini ya msanii mkongwe wa muziki huo nchini Joseph Haule"Profesa Jay"

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
Wangoto Click - kuwaonyesha Mitaa ya Home kwenye Video

KUNDI la muziki wa hiphop la Wangoto Click lenye maskani yake Temeke,Dares
Salaam,Tanzania limekamlisha kazi ya kurekodi video yake ya kibao chake
kipya Mitaa ya home ambacho kimejipatia umaarufu katika ulimwengu wa muziki
nchini.

Akizungumza na Mtandano huu,mmoja wa wasanii wa kundi hilo,Abdul Ally"Mzim"
alisema kibao chao hicho kimefanyiwa shooting na kampuni ya TMK
Production,baada ya kuonekana kupendwa na wengi.

Alisema mbali na kufanyia shooting kibao hicho,pia kundi lake ambalo
linaundwa na wasanii wawili,yeye na Abdul Bakari"Malipo"wametoa kibao chao
kipya ambacho ni cha tatu kilichobeba jina la Kipi alichopenda
wakimshirikisha Msanii Chegge toka kundio lao la Wanaume Family.

Mzim alisema hatua ya kutoa vibao hivyo ni kuelekea kutoa albamu ya kundi
lao,ambalo ni sehemu ya kundi la Wanaume Family.

"Wengine walijua kundi letu limekufa,hivyo tunataka kutoa albamu ili
kuonyesha bado tupo" alisema Mzimu.

Nyimbo ambazo zimetolewa na kundi hilo ni tatu ambazo ni Tutatawala
wakimshirikisha msanii Ray C,Mitaa ya home na Kipialichokipenda
walivyomshirikisha msanii Chegge toka kundi lao la Wanaume Family.
 
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
August 01, 2005
 
Makala ya James Nindi

 

 Makala na James Nindi - Kuhusu muelekeo na mtazamo wa HIP HOP , Tanzania

 

Nafikiri nitaanza kuandika kwa kuanzia na mawazo ambayo nilipata kuyasikia katika siku za nyma juu ya muiziki huu.
 
Mara ya kwanza pale ambapo muziki huu ulianza mwanzoni mwa miaka 90,jamii kubwa iliuchukulia muziki huu kama ni uhuni.
 
Kutokana na hilo sehemu kubwa ya  jamii hapa Tanzania,hasa watu wenye umri kuanzia miaka 45 kwenda juu waliuchukulia

muziki huu kama ni uhuni na hauna faida yoyote ka vijana wao. Hivyo walipoanza kuupiga vita,wapo vijana ambao

walikuwa na uwezo wa kufanya hiphop alisi kwa kipindi hicho walishindwa kuendelea kutokana na vita kubwa toka kwa

 wazazi wao. Hali hiyo iliweza kuendelea na kulianza kutjitokeza mapinduzi,baada ya baadhi ya wasanii kuanza kutoa

nyimbo ambazo zilikuwa zimebeba ujumbe mzuri kukemea mazovu kama,Mabaya ambayo yanatokea katika miji, mfano

walitoa nyimbo kutahadharisha mambo mabaya katika Jiji la Dar es salaam.Umalaya,Wanasiasa wabaya na kero nyingine.

 
Hali hii iliweza kuwavuta baaadhi ya waze kuanza kuwa na mtazomo tofauti katika muziki huu,mbali na kuvutiwa na ujumbe

 wa baadhi ya wasanii,pia muziki huo ulianza kutoa ajira kwa vijana wengi.

 
Mfano vijana ambao hawakupata nafasi za kuendelea na masomo yao,waliweza kupata nafasi ya kushiriki katika muziki

huo na kuweza kujiendeshea maisha yao na kuzisupoti familia zao.

 
Hili lilizidi kuongeza imani kwa wazee wengi kuupenda muziki huu,hivyo kadri siku zilivyokwenda muziki huuuliendela

kupata sifa kiasi cha hata wanasiasa wakubwa akiwem rais Mkapa aliwahi kunukuu maneno ya Msanii Joseph Haule

kutoka katika kibao chake,Ndiyo Mzee ambapo alikuwa anawashutumu wanasiasa waongo.

 
Mbali na kuonyesha mafanikio hayo katika siku za nyuma,pia muziki huo umeonyesha kuwa na mapungufu katika siku za usoni.
 
Mapungufu hayo ni kama Kokosekana ubunifu,Nyimbo nyingi kufanana kwa ujumbe au ala,wasanii wao kutokuwa

na umoja na pia wamekuwa wakiigfa sana kutoka nchini za magharibi likiwemo hata suala la mavazi.

 
Hilo linaweza kuleta athari kubwa sana kwa upande wa utamaduni,maana wasanii wamekuwa wakikiuka kabisa asili zao.
 
Kwa sasa,baadhi ya wazee tena wameanza kuupa kisongo muziki huo kutokana na mambo yanatofanywa na

baadhi ya wasanii wake.Ni jambo la kawaida kwa sasa kukukata na kijana,msanii fulani amevaa hereni na amesuka

 nywele kama msichana. Hivyo baadhi ya wazee tena ambao walikuwa wapenzi wa muziki huo,kwa kushiriki katika

matamsha na kununua kazi za wasanii hao wameacha hilo kwa kuona wasanii wanapotoka..

 
Nafikiri wanahitajika kupata semina za mara kwa mara ili kuweza kujua miiko ya muziki huo ili iweze kuwasaidia

 kujua njia za kupita kwani wengi wao walianza vizuri.

 
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
July 30, 2005
 
Dondoo za Bongo
na James Nindi, Tanzania
 

Stara ana wasiwasi na mapenzi

MSANII mahiri wa muziki wa Zouk nchini Tanzania,Stara Thomas yupo mbini

kutoa video yake mpya ya kibao Wasiwasi wa Mapenzi ambayo imerekodiwa

na kampuni ya Visho Lab ya ijini Dar es Salaam Tanzania.

 
Akizungumza na Mtandano huu,Dar es salaam juzi,Stara alisema kazi ya kurekodi

kanda hiyo imefanyika chini ya kampuni hiyo kwa ustadi wa hali ya juu.

 
Msanii  huyu ambaye ametamba na vibao vyake kadhaa kikiwemo

Mimi na wewe,alisema wimbo huo umerekodiwa katika studio za Akili's,

zilizopo,Ilala,Dar es salaam,Tanzania.

 
Stara msanii wa kike ambaye anauwezo mkubwa wa kujiamini,alisema mara

baada ya kazi hiyo kukamilika,inatarajiwa kusikia na kuonekana katika vituo

 vya luninga nchini Tanzania mapema mwezi Agosti.

 
Hata hivyo msanii huyu alisema hiyo ni njia ya kuanza kuandaa albamu

yake mpya ambayo itabeba nyimbo kadhaa na atazidi kuizungumzia kadri siku zinavyosonga mbele.

 
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Big Dogg Posse kuonekana - Kona Zote ndani ya album mpya

 
KUNDI la muziki wa hiphop la Big Dogg Posse(BDP- Kamili )la nchini hapa

linajiandaa kufanya uzinduzi albamu yake mpya,Kona Zote" 

baada ya kuingiza katika soko la muziki nchini.

 
Akizungumza na Mtandao huo,Dar es Salaam jana,Kiongozi wa kundi hilo,Drezy Chief

alisema mara baada ya kazi ya kuingiza sokoni albamu yake kukamilika,sasa hivi kundi

hilo linajiandaa na uzinduzi.Alisema kutokana na kazi hioyo kupenda na wengi,bado kundi

lake linajiandaa na kufanya hilo kutokana na kpata mialiko mingi katika mikoa mbalimbali

 wakitaka uzinduzi huo ukafanyike.Mbali na kujiandaa na hilo,alisema video yao,Kona zote

ambayo imefanya na kampuni ya Roca Production ya jijini Dar es salaam.

Tanzania,imekuwa ikifanya vizuri katika soko la muziki kutokana na kupendwa na wengi.

 
"Bado hatujaingia mkanda wetu wa video sokoni,ila wimbo huu unatakiwa na wengi

tuuingize kaa single yetu katika video" alisema msanii huyo. Albamu hiyo ya klona zote

imebeba jumla ya nyimbo nane ambazo ni,mama,Changu,Walimwengu,

Kwenye pati,Maimuna,kwenye 18, na wamewashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo

Bizzman,Mac 2b,Q-chief pamoja na Enrico toka katika studio za Sound Crafters

za Jijini Dar es Salaam.Tanzania. Kundi hilo kwa sasa limejipatia umaarufu mkubwa

hapa nchini kutokana na kibao chake hicho Kona zote kutamba katika vituo mbalimbali vya redio.

 
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Kala P awapinga mizinga wenye luninga

 
KUNDI la muziki wa Hiphop la Kikosi cha Mizinga lenye maskani yake block 41,Kinondoni,

Dar es salaam,Tanzania limelalamikia kitendo cha vituo vya luninga nchini Tanzania kutoipa

kipaumbela video yao mpya,Mstari wa mbele.

 
Wakizungumza na Mtandano huu,dar es salaam,kiongozi wa kundi hilo,Kalla Pinna alisema

pamoja na kibao chao hicho kushika nafasi za juu katika vituo vya nje,bado vituo vya hapa

havionyeshi ushirikiano na kundi lake. Alisema kibao chicho ambacho kimerekodiwa na

kampuni ya Kikosi Production yenye maskani yake,Italy kimeshika nafasi za juu katika kituo

cha television cha channel O,cha Afrika Kusini,ila hapa nchini hakipati nafasi hata kuingia Top Ten.

 
Alisema hali hiyo inatokana na baadhi ya watangazaji wa vituo vya televisheni kutofanya

 kazi kwa haki na kuweka mbele masuala ya rushwa. "Sisi hatupo tayri kutoa rushwa kwa ajili ya

 kazizetu zipate nafasi,ila ubora wetu wa kazi wananchi wanaufahamu" alisema kiongozi huyo.

 
Akizungumzia mikakati ya kundi lake,alisema lipo mbioni kufanya uzinduzi wa albamu yake,

Kufa au kupona ambayo imekamilika kurekodiwa katika studio za Bongo Records

 chini ya produza P.Funk

  
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Mazimwi - GWM kutoka na moto mkali

 
RASHID Ziada msanii wa kundi kongwe la Gangster With Matatizo(GWM)

laenye maskani yake Temeke,Dar es Salaam,Tanzania alisema pamoja na yeye kuwa katika kundi

la wanaume Family badop kundi lake hilo lipo. Akizungumza na Mtandano huu Dar es Salaam,

Tanzania,Rashid maaraufu kama Kr alisema kuwa kuwa kundi lake hilo ambalo limeudwa na

 wasanii wawili,yeye na D Chief bado lipo na linajiandaa kutoka  na moto mkali.

 
Alisema katika kudhihirisha hilo,tayari kundi lake limeanza kazi ya kutambalisha vibao vyake

vipya ambavyo vimeanza kusikika katika vituo vya redio.

 
"Tumeanza kutoa nyimbo zetu kama Nyumbani ni Nyumbani ambayo inaonyesha kupendwa

na wengi" alisema msanii huyo.

 
Alisema kinachochelewesha kundi lake kutoa albamu yake ni kutokana na mfumo uliopo

 katika kundi lao la sasa loa kupeana nafasi. Kundi hilo ambalo ni moja kati ya makundi

makongwe nchini liliwahi kutyamba na vibao vyake kadhaa kikiwemo Yamenikuta ambapo

 walimshirikisha mmoja wa wasanii wa muziki huo wakongwe nchini Tanzania,Joseph Mbilinyi.

 
Aidha Kr alisema katika albamu yao mpya ambayo itakuwa ya pili,itabeba mchangiko

wa nyimbo zikiwemo hata reggae na hilo ni kutaka kuionyesha jamii kwamba wao ni wakali.

 
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
July 24, 2005
 
Dondoo za Bongo
na James Nindi, Tanzania
 
Joan Matovolwa kutowa album - 'Maana ya Love'

MSANII wa kike wa muziki wa Zouk na RnB,Joan Matovolwa amesema yupo mbioni
kutoa albamu yake itakayojulikana kwa jina la Maana ya Love.

Msanii huyu ambaye alipata sifa nyingi baada ya kushirikishwa na
msanii,Dataz katika kibao chake cha Mume wa Mtu,alisema tayari kazi hiyo
ameianza ambapo kibao chake "Unastahili" kimekamilika kurekodiwa na kimeanza
kusikika katika vituo vya redio nchini.

Alisema baada ya kibao hicho kukamilika,bado anaendelea na kazi ya kurekodi
albamu yake hiyo kwa kuzitumia studio za Akil's Records,Backyard pamoja na
studio za FM zote za Jijini Dar es Salaam.

Mbali na hilo,msanii huyo ambaye nakuja juu katika muziki huo katika siku za
karibuni,alisema ndani ya albamu hiyo atawashirikisha wasanii kama
D-Knob,Pauline Zongo,Spider toka kundi la Mambo Poa na msanii Akil the
Brain.

Hii ni albamu ya kwanza kwa msanii huyu ambaye ameshirikishwa katika kazi za
wasanii mbalimbali kutokana na kuonekana anauwezo mkubwa.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Danny anavyo Hisi ndani ya video mpya
 
DANNY Msimamo msanii wa muziki wa hiphop toka mkoani Tanga ambaye anatamba
na wimbo wake MIC, amesema anajiandaa na kazi ya kurekodi video yake ya pili
ambayo inaitwa Nahisi.

Katika mahojiano na mtandano huu,Dar es salaam ,Tanzania juzi,Msimamo ambaye
 amejipatia sifa kwa ajili ya wimbo wake huo na video ya wimbo wake huo
alisema amefikia uamuzi ili kuweza kuzidi kujitangaza.

Alisema baada ya kukamilisha kurekodi albamu yake hiyo mjini Tanga katika
studio za Motika,ameanza kazi ya kurekodi nyimbo zake zote katika mkanda wa
video ili aweze kuingiza albamu ya video siku chache zijazo.

Aidha Danny alisema albamu yake hiyo,Mic imebeba jumla ya nyimbo nane na
amewashirikisha wasanii wengi toka kona mbalimbali nchini.

Aliwataja wasanii ambao wameshirikisha katika albamu yake hiyo kuwa ni
pamoja na Freddy Maliki "Mkoloni" toka kundi la Wagosi wa Kaya lenye maskani
yake mjini Tanga,Dj Scratch toka Mjini Tanga,Kado,Advocate pamoja na Dami K.

Aidha msanii huyo ambaye anazidi kupanda chati kila siku,amesema kazi ya
kurekodi albamu hiyo katika mkanda wa viodeo inatarajiwa kufanywa na kampuni
ya Wananchi ya jijini Dar es salaam,Tanzania.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Majitu - LWP wafanya mamboz Soundcrafters- kuna kitugani kipya?

KUNDI la muziki wa Hiphop la Live with Purposse( LWP-Majitu) majitu lenye
maskani yake Temeke,Dar es salaam -Tanzania limesema lipo
studio,Soundcrafters,likiwa linaendela na kazi ya kurekodi albamu yake ya
pili.

Wakizungumza na Mtandano huu,wasanii wa kundi hilo,walisema tayri kazi hiyo
imeanza na kibao.Shagwe na vigelegele kimekamilika kurekodiwa na kimeanza
kusikika katika vituo vya redio nchini Tanzania.

Mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo,Rock Clement."Rockmen"alisema kazi
hiyo inakwenda vizuri na albamu hiyo inatarajia kubeba jumla ya nyimbo nane.

Alisema hatua hiyo inakuja baada ya kundi lake kupata mafanmikio makubwa
kupitia albamu yake ya mwanzo,Mke wa mtu sumu" na hivyo kupokea maombi mengi
wakitakiwa kutoa albamu mpya.

Alisema kazi hiyo inatarajiwa kufanyika kwa umakini mkubwa ili kuifanya
albamu hiyo kubwa bora zaidi.

Kundi hilo limeundwa na wasanii kadhaa wakiwemo,Issa Iddy"slowter"Ally
Khamis"Doax Make".

Msanii huyo alisema mara kazi ya kurekodi albamu hioyo itakapokamilika
,wataendela na kazi ya kurekodi video ya albamu hiyo.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
July 23, 2005 - New York, New York
 
Balozi Dola ndani ya Movie ya Hip Hop - 'Bongo Barber's Shop'

Msanii machachari wa Hip Hop Balozi Dola anoishi na kufanya
shughuli zake za Hip Hop mjini New York, USA amekamilisha
kushooti Video ya Hip hop na kupiga hatuwa yaki historia katika Bongo
flava kwa kuwa msanii wa kwanza toka Africa kurekodi Cinema fupi ya
Hip Hop na wa asisi na ma gwiji wa sanaa ya rap.
 
Cinema hiyo imerekodi Bronx, New York na Director ano heshimika katika
kutengeneza cinema za Hip Hop Charlie Ahearn. Charlie amewahi
kutengeneza cinema iitwayo 'Wild Styles', mwaka 1982 inajulikana kama
movie kali sana inoelezea chimbuko la Hip Hop na kuelezea sanaa hiyo
ilivyoanza Marekani.

Cinema ya hivi sasa na Balozi Dola imewahusisha wakina Grand Master
Caz (Wa Cold Crush Brothers), DOA (Mtalaam wa kupiga beat kwa mdomo) ,
DJ EZ Mike ambaye ni katika ma DJ wa kwanza wa Hip Hop na Grand Wizard
Theodore ambaye ni mtu aliye buni sanaa yakusuguwa santuri (LP) na
shindano. Cinema hiyo inatumia kiswahili na Kingereza katika upande wa
mashahiri. Imerekodiwa kwenye nyumba ya kinyozi (Bronx, Headquaters)
karibu na Hip Hop ilipoanzia.

Cinema hiyo ' Bongo Barber's Shop ' iko katika hatuwa zakufanyiwa
ukarabati wa mixing na editing na inatarajiwa kutoka mwezi wa Agosti
mwanzoni. Itaonekana katika stesheni kama BET, VH1, Channel O , MTV2
,na kwa upande wa Tanzania ITV, DTV, TVT, TVZ, Start TV, Abood TV

Pia Balozi Dola yuko mbioni kutowa CD mchangayinko ya Bongo Flava ya
kwanza Marekani inojumuisha wasanii mbali mbali toka Tanzania, Ulaya
na Marekani kutambulisha kwenye soko la dunia. Tayari amesha fanikiwa
kupata mkataba wa usambazaji Marekani na Ulaya nzima - kwa masanii
ambayo wana taka kupata nafasi yakuwa kwenye toleo lijayo wasilisha
kazi yako kwa Kebby na Jerry kama nyimbo imekubalika tunaweza kusign
mkataba wa usambazaji na wewe.

Kwa wasanii wanopenda kuwa kwenye CD mchanganyinko wasiliana na balozi
kwa njia ya email: balozi@kwetuentertainment.com
 
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
Balozi ahojiwa na BET, New York , New York

Balozi Dola's interview on BET. COM click on icon to read more

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Dondoo za Bongo

 na James Nindi, Tanzania

 July 20, 2005

Mheshimiwa Temba (Wanaume Family)

MSANII mahiri wa muziki wa hiphop Amani Temba a.ka. Mheshimiwa Temba toka

kundi la Wanaume Family lenye maskani yake Temeke,Dar es Salaam amesema

ameanza kazi ya kurekodi albamu yake ya pili itakayojulikana kwa jina la "

Ipo siku".

Akizungumza na Mtandano huu mjini Dar es Salaam Tanzania hivi

karibuni,msanii huyo alisema kazi ya kurekodi albamu hiyo ambayo itabeba

jumla ya nyimbo kumi imeanza.

Alisema tayari nyimbo mbili,Kosa la Baba na namshukuru zimerekodiwa katika

studio za Sound crafters na Aegies zikiwa ni sehemmu ya utangulizi.

Msanii huyu ambaye anatamba na albamu yake ya kwanza,Umasikini Jeuri alisema

katika albamu yake hii ya pili anatarajia kuwashirikisha wasanii kadhaa toka

kundi lake la Wanaume family akiwemo Juma Nature,Chegge na Luteni Karama.

Mbali na kuwashirikisha wasanii hao toka katika kundi lake,pia alisema

anatarajia kuwashirikisha wasanii wengi toka nje ya kundi hilo ambao bado

anafanya nao mazungumzo.

Temba alisema kazi ya kurekodi albamu hiyo inatarajiwa kuendelea na albamu

hiyo inatarajiwa kupataikana katika soko la muziki mwanzoni mwa mwaka ujao.

Aidha akizungumzia ju ya muziki wa hiphop nchini,alisema muelekeo wake ni

mzuri kutokana na idadi ya wasanii wenye uwezo kujitokeza kwa wingi.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Wagosi wa Kaya - Kuzinduwa album 'Nyeti"

KUNDI la muziki wa Hiphop la Wagosi wa Kaya lenye maskani yake mjini Tanga

limekamilisha kazi ya kurekodi albamu yake mpya ya nne iliyobeba jina la

Nyeti katika studio mpya za kisasi za Aegies zilizopo Mikocheni,Dar es

salaam, Tanzania.

Wakizungumza na Mtandano huu katika studio hizo hivi karibuni,Dar es salaam

wasanii wanaounda kundi hilo,Freddy Maliki a.k.a Mkoloni na John Simba a.k.a

Dr John walisema wamekamilisha kazi ya kurekodi albamu hiyo ambayo imebeba

jumla ya nyimbo nane.

Walisema mara baada ya kukamilisha kurekodi albamu hiyo wametoa kibao chao

Nyeti katika vituo mbalimbali vya redio ili washabiki wao waweze kukisikia.

"Sasa hivi tunajiandaa kunza kazi ya kurekodi mkanda video wa albamu yetu

hii ili tuendelee na masuala mengine" alisema Mkoloni.

Aidha Dr John alisema albamu yao hiyo imebeba vibao kama kiinua

mgongo,Taarifa ya habari,Zawadi,Pole,Mjenga nchi mwananchi, Acha kujiuliza

na kile kilichobeba jina la albamu hiyo Nyeti.

Wasanii hao walisema katika albamu hiyo wamewashirikisha wasanii kama Danny

Msimamo amnayetamba na kibao chake cha Mic na msanii chiopukizi Tecla.

Kundi la Wagosi wa kaya ni moja kati ya makundi ya muziki nchini Tanznia

lenya sifa kubwa ya kutunga nyimbo zenye ujumbe mkali wa kuikosoa Serikali

na viongozi ambao wanashindwa kuwajibika.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

East Coast Team

KUNDI la Muziki wa hiphop la East Coast Team lenye maskani yake

Upanga,Jijini Dar es salaam Tanzania linatarajia kufungua kampuni ambayo

itahusika na uuzaji wa kazi zao katika siku za mbeleni.

Kiongozi wa kundi hilo,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy GK alisema kuwa

hatua hiyo imefikiwa na kundi lake ili kuweza kuepukana na wimbo wa wizi wa

kazi za wasanii.

Alisema kampuni hiyo katika hatua za mwanzoni itahusika na uuzaji na

usambazi wa kazi za wasanii wa kundi lake duniani kote na baada ya kupata

uwezo zaidi litaingia mikataba na wasanii ambao watapenda kufanyiwa hivyo.

King Crazy GK alisema kwa sasa kundi lake lipo katika hatua za mwishoni ili

kuweza kuanza kazi hiyo ambapo vitu kama flana,kofia,chupi,soksi,jeans,kanda

video za albamu,kanda,VDC,DVD za wasanii wa kundi hilo zitauzwa.

Alisema mbali na kusimamia kazi za uuzaji huo,pia kampuni hiyo itaweza

kuwatafutia wasanii wake masoko ya nje kwa ajili ya kufanya matamasha

mbalimbali ambayo yataonekana kuwa na maslahi kwao.

Kundi la East Coast limeundwa na wasanii wengi wakiwemo,Ambene Yessaya AY,

Benjamin Gembe,Buff G,Pauline Zongo,Khamisi Mwinjuma "Mwanafalsafa" Adamu

Snare,Gwamaka Kaihula "King Crazy GK" na wengineo

 Bonyeza hapa kutembelea tovuti ya East Coast Team ( ECT )

Back to Home page